Wednesday, 30 December 2009

Kiswahili Wikipedia Challenge spurs local online content in Africa

En Français

‘Local content’ can be defined as the expression and communication of a community’s local ideas, knowledge and culture, often times in their own language. Global or non-local content tend to reflect language, values and lifestyles that are vastly different from those of the community "consuming" the content. As the use of the Internet and its resources spread, it is becoming increasingly clear that in order to promote greater access to information and to ensure Africa's active and inclusive participation in the development of information society, it is important to have more online content in local African languages. In addition, the global online community can benefit greatly from having access to Africa's rich cultural diversity and heritage.

Over the last 10 years, Google has been part of the Search journey for many growing regions and countries, helping to localise and provide access to information. Today, we are excited to be sponsoring the Kiswahili Wikipedia Challenge to encourage the creation of locally relevant online content in Africa. So, what is the Kiswahili challenge about? The Kiswahili Wikipedia Challenge is your opportunity to bring Africa's information online by creating Wikipedia articles in Kiswahili. As many of you well know, Wikipedia is an online collaborative encyclopedia that has become often referenced source of online information. While many people on the internet in Africa are fluent in English, French, Portuguese, etc., there are approximately 50-100 million Kiswahili speakers in East Africa and beyond and who aren’t yet on the internet but will be down the road. We hope to enrich and enhance the quantity and quality of local content online through the efforts of the community members. Kiswahili Wikipedia Challenge is small step towards that effort.

On December 14th, the interim prize winners were announced. They are the top contributors among the 800 individuals who signed up to take part in this Kiswahili Wikipedia Challenge. This challenge is still ongoing until January 2010 and is open to anyone who is passionate about creating Wikipedia articles in Kiswahili by translating via Google Translator Toolkit, existing Wikipedia articles or creating a new article from scratch. Qualifying winners will have a chance to win wifi internet ready laptops, netbooks, cellphones, etc. More information is found on the Kiswahili Wikipedia Challenge website.

Congratulations to the winners and we invite you to join them in the effort to contribute local content in arenas such as Wikipedia, where information is shared and used towards empowerment across the globe.

Here is the list of Interim Prize winners:

Jomo Kenyatta University of Agriculture and Technology (JKUAT) - Limoke Oscar
Strathmore University - Mark Ekisa
University of Nairobi - Peter Kamero
Institute of Finance Management (IFM) - Janeth Jonathan



====

Shindano la Wikipedia kwa Kiswahili lachochea maudhui ya kienyeji kwenye wavuti Afrika

‘Maudhui ya kienyeji’ yanaweza kufafanuliwa kama udhihiri na uwasilishi wa mawazo, ujuzi na utamaduni wa jamii ya eneo fulani, haswa katika lugha ya jamii hiyo. Maudhui ya kimataifa au yasiyo ya kienyeji mara nyingi huonyesha lugha, maadili na mitindo inayotofautiana sana na ile ya jamii inayopokea maudhui hayo. Kadri wavuti na nyenzo zake unavyokua, ndivyo inavyodhihirika kuwa ni muhimu kuwa na maudhui zaidi katika lugha za kiafrika kwenye wavuti, ili kurahisisha upati wa maarifa na kuhakikisha kuwa Afrika inashiriki kikamilifu katika ukuzaji wa jumuiya ya maarifa. Vilevile, jumuiya ya wavuti ulimwenguni kote inaweza kufaidika pakubwa kutokana na utofauti na utamaduni wa Afrika.

Katika miaka kumi iliyopita, Google imeshiriki katika safari ya Utafutaji katika maeneo mengi yanayokua, ikasidia kutafsiri na kuwezesha watu kupata maarifa. Ni furaha yetu kudhamini Shindano la Wikipedia kwa Kiswahili ili kuhimiza uundaji wa maudhui ya kienyeji yanayofaa kwenye wavuti Afrika. Shindano hili linahusu nini? Shindano la Wikipedia kwa Kiswahili ni nafasi yako kuleta maarifa ya Afrika kwenye wavuti kwa kuunda makala ya Wikipedia kwa Kiswahili. Kama wengi wenu mnavyojua, Wikipedia ni kamusi elezo ya ushirika kwenye wavuti, inayorejelewa sana kama chanzo cha maarifa. Ijapokuwa watu wengi Afrika wanaweza kusema kwa Kiingereza, Kifaransa, Kireno, n.k., kuna takriban watu milioni 50-100 Afrika Mashariki na kwingineko wanaozungumza Kiswahili, ambao bado hawako kwenye wavuti, lakini watakuwepo katika siku zijazo. Tunazimia kukuza idadi na ubora wa maudhui ya kienyeji kwenye wavuti kupitia jitihada za wanajamii. Shindano la Wikipedia kwa Kiswahili ni hatua ndogo katika jitihada hizo.

Washindi wa awamu ya kwanza walitangazwa tarehe 14 Desemba. Wao ndio wachangiaji wakuu kati ya watu mia nane waliojisajili kushiriki katika Shindano la Wikipedia kwa Kiswahili. Shindano lingali linaendelea hadi mwishoni mwa Januari 2010, na liko wazi kwa yeyote aliye na shauku ya kuunda makala ya Wikipedia kwa Kiswahili, kwa kutafsiri makala zilizopo kupitia Google Translator Toolkit au kuandika makala mpya kutoka mwanzo. Washindi watakaofuzu watapata nafasi ya kushinda kompyuta, kompyuta ndogo, simu za mkononi, n.k. Maelezo zaidi yanapatikana kwenye tovuti ya Shindano la Wikipedia kwa Kiswahili.

Hongera kwa washindi, na tunakualika ujiunge nao katika jitihada za kuchangia maudhui ya kienyeji katika ukumbi wa Wikipedia, ambapo maarifa hushirikiwa na kutumiwa ulimwenguni kote.

Hii hapa orodha ya washinidi wa awamu ya kwanza:

Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta (JKUAT) - Limoke Oscar
Chuo Kikuu cha Strathmore - Mark Ekisa
Chuo Kikuu cha Nairobi - Peter Kamero
Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) - Janeth Jonathan

Imechapishwa na Christine Moon, kwa niaba ya timu ya Shindano la Wikipedia kwa Kiswahili

====

Le "Kiswahili Wikipedia Challenge" stimule la création de contenu local en ligne en Afrique
​​
La notion de "contenu local" peut être définie comme l'expression et la communication des idées locales, du savoir et de la culture d'une communauté, le plus souvent dans la langue locale. Le contenu dit global ou non-local tend à refléter une langue, des valeurs et un style de vie qui peuvent être considérablement différents de ceux des communautés qui vont "consommer" ce contenu. Avec l'expansion de l'internet et de ses usages, il devient évident que, dans le but de promouvoir un meilleur accès à l'information et d'assurer une participation active et à part entière du continent africain au développment de la société de l'information, il faut mettre en ligne plus de contenu dans les langues locales africaines. En outre, ceci permet aux communités globales en ligne de bénéficier d'un accès privilégié à la richesse de la diversité culturelle et de l'héritage du continent africain.

Au cours de ces dix dernières années, Google a pris une part active à cette Quête (Search journey), pour de nombreuses régions et pays en développement, en aidant à la localisation et en facilitant l'accès à l'information. Aujourd'hui, nous sommes fiers de sponsoriser le Kiswahili Wikipedia Challenge, qui a pour but d'encourager la création de contenu localisé, pertinent pour le continent africain. De quoi s'agit-il ? Le Kiswahili Wikipedia Challenge est l'occasion de mettre en ligne l'information liée continent africain par le biais de la création d'articles Wikipedia écrits en Kiswahili. Comme beaucoup d'entre vous le savent déjà, Wikipedia est une encyclopédie collaborative en-ligne qui est devenue la référence de-facto pour l'information en-ligne. Même si de nombreux internautes africains parlent courament anglais, français ou portugais, il y a également entre 50 et 100 millions de personnes parlant Kiswahili en Afrique de l'Est et au delà. Ces personnes ne sont pas encore des internautes, mais vont bientôt le devenir. Et nous espérons pouvoir enrichir et améliorer -- en quantité et en qualité -- le contenu local mis en ligne, grâce aux efforts des membres de cette communauté. Le Kiswahili Wikipedia Challenge est une modeste première étape dans cette direction.

Le 14 Décembre dernier, nous avons annoncé les noms des vainqueurs provisoires : il s'agit des plus gros contributeurs, parmi les 800 participants qui se sont inscrits et ont participé au Kiswahili Wikipedia Challenge. Mais la "course" n'est pas terminée (vous avez jusqu'à fin Janvier 2010); elle reste toujours ouverte à ceux et celles qui sont passionnés par la création d'articles Wikipedia en Kiswahili soit en traduisant un article existant (par exemple en utilisant le Google Translator Toolkit), soit en créant de toutes pièces un nouvel article. Les vainqueurs auront une chance de gagner des ordinateurs portables wifi, des ultra-portables, des téléphones mobiles, etc. Pour plus d'information, rendez vous sur le site du Kiswahili Wikipedia Challenge.

Nous adressons nos félications aux vainqueurs provisoires et nous vous invitons tous à vous joindre à leurs efforts pour la création de contenu local sur des sites comme Wikipedia, où l'information est partagée pour que tous en bénéficient.

Voici la liste des vainqueurs provisoires :

Jomo Kenyatta University of Agriculture and Technology (JKUAT) - Limoke Oscar
Strathmore University - Mark Ekisa
University of Nairobi - Peter Kamero
Institute of Finance Management (IFM) - Janeth Jonathan

No comments:

Post a Comment